JINSI YA KUANDAA MPANGO BIASHARA (BUSINESS PLAN) ULIO BORA ILI UFANIKIWE
Imeandikwa Na Frank Mahamila
(Mtaalam na Mshauri wa Masuala ya Biashara na Uongozi wa Biashara)
Watu wengi kwa karne ya sasa huishi kwa
malengo ya kuwa watu fulani au watu wanaomiliki vitu fulani,yote hayo
yanaweza kufanikiwa endapo mtu/watu hao wapo tayari kufanya kazi kwa
juhudi na maarifa kwa kutumia viungo na akili zetu ambazo tumepewa bure
na Mwenyezi Mungu bila malipo yoyote.
Kutokana na changamoto tofauti tofauti
katika soko la ajira ikiwa sambamba na ufinyu wa upatikanaji wa ajira
zenyewe lakini pia maslahi duni, manyanyaso na mateso yanayopatikana
sehemu sehemu za kazi, watu wengi kwa sasa wanaona ni bora wafikirie
kuitwa WAAJIRI na si WAAJIRIWA tena.
Pamoja na matamanio hayo, watu wengi
wamekutana na changamoto kubwa katika kuanzisha au kuendeleza biashara
hizo. Naomba nieleweke wazi biashara si lazima kununua na kuuza,yaweza
kuwa ya kuzalisha na kuuza pia, hapa nazungumzia kujenga na kupangisha,
kulima na kuuza, utoaji wa huduma uliyosomea n.k.
Yote hayo na mengine mengi utafanikiwa
endapo tu utakuwa na MPANGO BIASHARA katika aina yoyote ya biashara
unayofanya au unayotaka kufanya. Mtandao huu kwa kutambua juhudi kubwa
za wasomaji wake kutaka kujikomboa kiuchumi leo tunakuletea jinsi ya
kuandaa MPANGO BIASHARA (BUSINESS PLAN) ILI UFANIKIWE. Huu utakuwa ni
mfululizo wa makala mbali mbali za UCHUMI NA BIASHARA PAMOJA NA FURSA
MBALI MBALI UNAZO WEZA KUZITUMIA HAPO HAPO UNAPOISHI.
UTANGULIZI
Mpango biashara Biashara ni nyaraka
muhimu sana kwa biashara yako kwakuwa inakupa picha ya matarajio ya
namna biashara itakavyokuwa. Ukifanya mchanganuo huo kwa ufasaha kama
inavyoelekezwa utaweza kutambua kama kweli biashara unayotaka kuifanya
itakulipa au la. Pia utaweza kutambua matatizo na changamoto kabla
haujaanza biashara.
Mpango Biashara kwa kiwango flani
unahitaji utafiti ili kuweza kuandika vema mambo yanayoendana na
biashara yako. Mfano unahitaji kufanya utafiti wa soko ili kujua kwa
biashara yako ni akina nani hasa watakuwa wateja wako, na kwanini
watakuja kununua bidhaa kwako. Pia unahitaji kufanya utafiti wa gharama
utakazotumia kuendesha biashara. Pia gharama za ununuzi wa samani pale
utapoendeshea biashara yako,kama Meza, Kiti n.k
Mpango Biashara unakuhitaji ujue picha
kubwa ya mazingira ya biashara yako pindi utakapoianzisha. Mfano masuala
ya Kodi, Masuala ya Kisheria kama vile Sheria za Ajira, Vibali,
Uendeshaji wa Biashara n.k.
Na mwisho kama unataka kuandika Mpango
Biashara ili ukaombe mkopo, basi fikiria kwa umakini namna ambavyo
utakuja kuulipa mkopo husika. Umejipangaje katika usimamizi makini wa
biashara yako.
Ufuatao ni mtiririko wa mchanganuo wa biashara.
Jalada la nje:
Linahusisha jina la biashara, muda wa mpango (mfano. 2016 – 2020),
anuani ya biashara, toleo, jina la aliyeandaa, mwaka pamoja na kuonyesha
mchanganuo unaelekezwa kwa nani.
Dibaji: Sehemu hii
huandikwa muhtasari wa mambo mbalimbali yaliyoanishwa katika mchanganuo
mathalani, aina ya biashara, bidhaa au huduma zinazotolewa kwa ufupi,
mpango wa mauzo, mpango wa ukuaji kwa mwaka, soko lengwa, mtaji
unaohitajika, namna mwekezaji au mdau anavyoweza kunufaika iwapo
akiwekeza au benki ikikupatia mkopo namna gani utalipa.
Maelezo ya biashara:
Dira/ndoto, madhumuni, historia fupi ya biashara, bidhaa au huduma
inayotolewa kwa mapana, uchanganuzi wa hali ya tasnia kwa sasa na siku
zijazo, uchanganuzi wa hali ya biashara kwa kuainisha upungufu na nguvu
ndani ya biashara, fursa na vihatarishi katika mazingira yanayoizunguka
biashara.
Masoko: inazungumzia
hali ya soko katika tasnia ya biashara husika, soko unalopanga kuuzia
bidhaa au huduma, unaweza kuchukua nafasi gani katika soko hilo kwa
asilimia.
Mbinu unazotumia kufikisha bidhaa au
huduma kwenye soko, mpango wa mauzo kwa mwezi, kwa mwaka hadi muda wa
mpango uliojiwekea mathalani miaka 3 hadi miaka 5, mpango wa bei, hali
ya ushindani, mbinu za kuendana na ushindani katika soko, namna ya
kutangaza biashara, na unapaswa kuangalia ni jinsi gani utaweka
kipaumbele katika kutangaza bidhaa kama una zaidi ya bidhaa moja.
Menejimenti na Utawala:
Mfumo wa biashara kama ni ya mtu mmoja, ubia au kampuni, chora chati ya
mtiririko wa madaraka, wasifu wa maofisa wa ngazi za juu mathalani
Mkurugenzi Mtendaji na wakurugenzi wengine, idadi ya wafanyakazi kwa
sasa, mpango wa ukuaji au kuongezeka kwa wafanyakazi, mfumo wa umiliki
kama ni kampuni-weka mchanganuo wa hisa za kila mmliki, kama ni ubia
elezea mchango wa kila mmoja na namna ya kugawana maslahi, toa
mchanganuo kwa wataalam mbalimbali unaowatumia katika biashara mathalani
mshauri wa biashara, mwanasheria, wasafirishaji na wakaguzi.
Masuala ya Fedha: Weka makisio ya mizania, mapato na matumizi na mtiririko wa fedha kwa muda wa mpango tangu sasa.
Maelezo ya dhana ya kifedha iliyotumika
kupanga makisio, muundo wa mtaji (ainisha kiasi cha mtaji binafsi,
msaada, mikopo, na njia nyinginezo kama zipo).
Mwisho ni mpango wa kupata fedha kama
zinatoka kwa wawekezaji au benki- kiasi gani unahitaji kwa muda gani na
namna gani utalipa kwa faida gani.
Mchanganuo wa vihatarishi vya biashara:
Ainisha vihatarishi vya biashara yako, fursa za kibiashara zinazoendena
na vihatarishi hivyo, mchanganuo wa itakuwaje endapo mipango
uliyojiwekea haitatekelezeka, mchanganuo vihisishi, kwa mfano namna gani
bei ikipanda au kushuka inaweza kubadilisha mwelekeo wa biashara yako.
Ratiba ya uzalishaji bidhaa au utoaji huduma: Mara nyingi ratiba ya uzalishaji inafanywa kwa programu za kinakilishi.
Viambatanisho:
Viambatanisho mbalimbali huwekwa kulingana na mtumiaji wa mchangunuo huo
mathalani wasifu binafsi wa maofisa wa ngazi za juu, nakala ya vyeti
vya usajili, TIN, leseni na vibali vya biashara.
KWA UFUPI VITU VYA KUZINGATIA KATIKA KUANDAA MPANGO BIASHARA
- Muhtasari wa biashara yako
- Historia na maelezo ya biashara yako
- Maelezo ya bidhaa au huduma ya biashara yako
- Mchanganuo wa masoko
- Ukubwa wa soko
- Mgawanyo wa soko
- Aina ya soko/masoko
- Mchanganuo wa ushindani
- Watoa huduma au wauza bidhaa kama yako
- Udhaifu wao
- Uwezo wao
- Mkakati wa utekelezaji
- Uongozi na usimamizi wa kazi
- Uchambuzi wa madhaifu, nguvu, fursa na hatari zinazokabili biashara yako
- Mkakati wa Uzalishaji
- Mkakati wa kuuza
- Mpango wa fedha
- Uchambuzi wa mahitaji ya mtaji
- Wapi utatoa mtaji
- Matumizi ya mtaji
- Makisio ya Mauzo
- Uchambuzi wa kurudisha gharama (break even analysis)
- Makisio ya faida au hasara
- Makisio ya mzunguko wa fedha katika biashara yako (cashflow)
- Makisio ya oanisho la mali na madeni ya biashara yako (balance sheet)
- Ulinganifu wa sehemu mbalimbali za biashara (business ratios)
-
- Leseni
- Cheti cha ulipaji kodi
- Cheti cha usajili
- Taarifa mbalimbali za biashara yako ambazo hazikupata nafasi ndani ya mchanganuo huu.
“MONEY IS AN IDEA YOU HAVE THEN YOU CONVERT IT INTO PAPERS”
Kwa maoni/ushauri :-
Barua pepe: duxmantwo@yahoo.com
Nashukulu sana kwa elim nzuri ya uwandishi lakini ninatatizo katika uwandishi kama mjuavyo kuandika maneno ya kuvutia nacho nikipaji je naweza kupata mtu wa kunisaidia kwani nina lengo la kufungua kampuni yangu binasi
ReplyDeleteNitafute nitakusaidia
DeleteTutafte pia tunafanya kazi hii.
DeleteEmail: danideoji@gmail.com
Hongera kazi nzuri nimejifunza kitu kutoka kwako, nami nachukua hatua ya kuandika mpango biashara wangu.asante sana.
ReplyDeleteThanks for briefly clarification.
ReplyDeleteStay blessed
Ahsante
ReplyDeleteThanks so much
ReplyDeleteAhsante Sana kwa somo zuri
ReplyDeleteHabari,naomba angalau sample ya draft inayoonyesha business plan
ReplyDeleteAsante kwa ufafanuzi ,naomba mfano wa wa business plan
ReplyDeleteWell.. Iko vyema
ReplyDeleteasante mkuu nimepata elimu
ReplyDeleteMsaada wa kuandaa business pln
ReplyDeleteNaweza pata copy ya business plan yeyote
DeleteKuandaa bado nishida kidg naweza kupata mfano wa business plan
ReplyDeleteNashukuru kwa mwongozo huu.
ReplyDeleteHabari za mchana naomba jedwali la biashara
ReplyDeleteNahitaji business plan ya KUKU PROJECT Itakayo jumuisha mashine ya kukoboa na kusaga ilinizalishe chakula mimi mwenyewe,incubater kwa utotoleshaji wa vifaranga ,ujenzi wa mabanda naana eneo la kuendeshea shughuli hii lipo lenye wastani wa hekari nane(8)Lengo kuu ni kuzalisha na kuuzaa kuku wa kienyeji na mayai ya kuku wa kienyeji,naomba maelekezo yako tafadhali.
ReplyDeleteGud, umesafiri kwenye hisia zangu! Mungu atupe ustamilivu zaid tunaoamini katka kufuga kuku... one love!,,
DeleteNashukur 🙏🏿
ReplyDeleteIko vyema itasaidia wengi, barikiwa. Ila wakitaka msaada zaidi husiwaache maana ni ukombozi huu toka ngazi ya kifamilia hadi taifa,nimeipenda kazi yako kiongozi
ReplyDeleteWow good idea and briefly clarification
ReplyDelete